Alhamisi
ya March 20 2014 lilitoka tamko ambalo lina maamuzi ya msanii wa
bongofleva Dogo Janja kuhusu kuomba msamaha na kuhitaji kurudi kwenye
kundi lake za zamani la Tiptop connection na kuyasahau yaliyopita kati
yake na aliyekuwa meneja wake pia ambae ni Madee.
baba mzazi wa Dogo Janja amepata nafasi kuzungumza kwa mara ya kwanza baada ya mtoto wake kuomba msamaha.
Anasema >>’Dogo Janja alishakua mtu mzima na tayari nilishawahi kumwambia achague mahali atakapoona kuna manufaa kwake, akishafanya
maamuzi yake huwa ananishirikisha kwenye kujadiliana, tayari alishawahi
kuniambia kuwa atafanya maamuzi baada ya kuona Mtanashati hakuna
muelekeo wowote na hakuna anachopata ndipo akaniambia baba mimi mtu
yoyote au kundi lolote nitakalokubaliana nalo basi nitafanya nao kazi’.
Hayo ni maelezo ya Baba mzazi wa Dogo Janja ambae ametoa baraka zote
kwa Janja kurudi kujiunga na Tiptop Connection hivyo kazi imebaki
kusikia kutoka upande wa Tiptop kufahamu kama wameukubali msamaha wa
Dogo Janja.
没有评论:
发表评论