2014年3月27日星期四

MAFIKIZOLO KUTUA BONGO DAR ES SALAAM MWEZI UJAO.



Kundi maarufu  la Muziki kutoka Afrika Kusini, Mafikizolo linatarajiwa kudondosha burudani ya aina
yake itakayoacha gumzo Jijini Dar es Salaam, katika ukumbi wa Mlimani City tarehe 5 mwezi Aprili mwaka huu, kwa ajili ya kuwapa burudani ya moja kwa moja wapenzi wa muziki wao hapa Tanzania.


Mafikizolo ambayo inaundwa na wakali Theo Kgosinkwe na Nhlanhla Nciza tayari wamejipanga vilivyo kwa ajili ya kulishambulia jukwaa katika onyesho ambalo linakuwa ni la kwanza kabisa kulifanya haba Bongo katika historia ya kundi hili.

Tiketi za onyesho hili linalosubiriwa kwa hamu, zinapatikana kwa shilingi 20,000 tu katika maeneo  na mlangoni siku ya tukio, tiketi hizi zitapatikana kwa shilingi 35,000.

没有评论:

发表评论