2014年3月25日星期二

Q CHILLAH; BADO NINAUWEZO MZURI WA KUIMBA HIVYO KUFANYA FILAMU SIO KUUKWEPA MUZIKI.


Mwimbaji wa bongo flava, Q Chillah ambaye hivi sasa anaonekana kuwa karibu zaidi na kiwanda cha filamu amesema kuwa kuingia kwenye tasnia hiyo haimaanishi kuwa amekimbia majukumu ya muziki.

Q Chillah ameiambia Bongo5 kuwa bado ana uwezo mzuri wa kuimba na ataendelea kufanya muziki na kwamba watu wanapenda afanye filamu japokuwa yeye sio mtu wa filamu.

“Japokuwa mimi sio mtu wa filamu lakini watu wengi wanapenda nifanye filamu. Kwa hiyo nashangaa baadhi ya watu wanadhani nimeenda kwenye filamu kwa ajili ya kuuza sura na kukimbia majukumu yangu ya muziki. Jamani mimi ni msanii mkubwa sana na nina uwezo mkubwa sana wa kuimba na kufanya vitu vizuri sana katika muziki.” Amesema Q Chillah.

“Kwa hiyo nitaendelea kufanya muziki wangu mzuri na kama nitahitajika kufanya filamu nitafanya. Lakini maisha yangu ya nyuma ya pazia naweza sana kufanya filamu vizuri sana, na pia si biashara.”

Ameeleza kuwa alifuatwa na JB na muongozaji Adamu Kuambiana wakamtaka afanya filamu ya ‘Hukumu ya Ndoa Yangu’ na kwamba JB alimwambia awe kwenye kampuni yake.

Source: Bongo5

没有评论:

发表评论