KIMEWAKA! Habari zilizothibitishwa zinaeleza kuwa, sura mbili za mauzo
kwenye sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu na Aunt Ezekiel Grayson
wanadaiwa kula kichapo kutoka kwa msanii mwenzao, Adam Kuambiana, Amani
limeinyaka.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na ‘shushushu’ wetu lilijiri mchana kweupe
maeneo ya Mikocheni, Dar, hivi karibuni baada ya kuibuka timbwili lenye
ujazo wa kilo kadhaa baina ya mastaa hao.
ALIANZA WEMA
Kwa mujibu wa chanzo, Wema ndiye aliyeanza kummwagia Kuambiana maneno ya
shombo akimwambia kuwa ahakikishe siku hiyo haipiti bila kukata kucha
za miguuni kwani ni ndefu na zinatisha.
“Mwanzoni ilikuwa kama utani tu. Wema alimwambia Kuambiana akate kucha,
tena itabidi atumie mkasi wa kukatia michongoma maana kwa wembe
hazikatiki.
“Pia Wema alimwambia yeye hawezi kumwacha mpenzi wake na kucha ndefu kama hizo za Kuambiana,” kilisema chanzo chetu.
Ilizidi kudaiwa kwamba wakati Wema akiendelea ‘kumpaka’ Kuambiana, Aunt
aliyekuwa amejilaza chini alidakia na kusikika akisema kuwa ni kweli
msanii huyo mwenye uwezo wa juu katika fani anatakiwa kukata kucha hizo
huku akizungumza maneno ya shombo kwa jamaa huyo.
HASIRA
“Baada ya kuona imekuwa ‘too much’, Kuambiana alipandwa na hasira,
akanyanyuka kwenye kochi na kumfuata Wema kwa lengo la kumpa kipigo,”
kilisema chanzo hicho.
MARTIN KADINDA AMUOKOA
Habari zilidai kwamba, Kuambiana alipomfikia Wema alianza kumpiga vibao
hadi meneja wake, Martin Kadinda akaingilia kati kumuokoa mwanadada huyo
ambaye pia ni meneja wake.
KIBAO CHAMGEUKIA AUNT
Chanzo kilieleza kwamba baada ya kuachana na Wema, msaanii huyo ambaye
pia ni ‘dairekta’ wa sinema mbalimbali za Bongo alimfuata Aunt na kuanza
kumlamba makofi ya kutosha.
Tukio hilo lilizua tafrani na kuwafanya wasanii wengine waliokuwa eneo
hilo wakimbie na kushindwa kuwatetea Aunt na Wema kwa kuogopa kugeuziwa
kibao.
KUAMBIANA ANASEMAJE?
Baada ya kuinyaka ishu hiyo, mapaparazi wetu walimtafuta Kuambiana na
kumuuliza kulikoni kugeuka bondia na kuwapiga warembo hao ambapo alikiri
kutokea kwa ishu huyo.
Alisema kuwa, Wema na Aunt ni kama wadogo zake, tena yeye kama dairekta wao walipaswa kumheshimu na siyo kumvunjia heshima.
“Akina Wema ni wadogo zangu, wanahitaji kuniheshimu na mimi ndiye
mwongozaji wa filamu yao, kwa nini wanikosee heshima? Hata kama
wamekasirika lakini nimewashikisha adabu,” alisema Kuambiana kwa ile
sauti yake nzito.
WEMA & AUNT
Kwa upande wao, walipoulizwa Aunt na Wema kuhusiana na kichapo
walichopewa walisema walishamzoea jamaa huyo, lakini kwa alilolifanya la
kuwapiga makofi aliwakwaza kwa sababu hata kama ni mwongozaji wa
filamu yao lakini alikuwa pale kwa ajili yao.
HISTORIA YA KUAMBIANA
Ukiachana na tuki hilo, Kuambiana anadaiwa kuwa na mkono mwepesi hasa
anapokuwa ‘lokesheni’ ambapo mwaka jana, aliwahi kumtia mikononi staa
mwingine wa filamu za Bongo, Rose Ndauka walipokuwa wakirekodi filamu
visiwani Zanzibar.
Siku ya tukio hilo, Kuambiana alikuwa akidairekti Filamu ya Distress in
Zanzibar. Alimshutumu Rose kuvaa mavazi tofauti na maagizo yake, katika
kujibishana akamuwasha makofi.
HATA MITAANI!
Juni, mwaka jana, Kuambiana alimshushia kipigo Fadhili Joseph ambaye
alimdai fedha za bia alizokunywa kwenye baa yake, Sinza, Dar es Salaam.
Kuambiana aliposhindwa kulipa aliacha laptop (kompyuta mpakato), siku
iliyofuata alirudi na kushusha kichapo huku akiitaka laptop hiyo.
Kuambiana alikamatwa na Polisi Kawe, Dar kwa faili la malalamiko
KW/RB/5761/2012 SHAMBULIO. Kesi hiyo ikahamishiwa Kituo cha Polisi
Kijitonyama ‘Mabatini’ kwa vile ndiyo kituo cha karibu na eneo la tukio.
MADAIREKTA WAKOJE?
Mbali na Kuambiana, staa mwingine ambaye pia ni dairekta wa muvi za
Bongo, Issa Musa ‘Cloud’ naye aliwahi kutoa kipigo cha bakora kwa msanii
Blandina Chagula ‘Johari’ kwa kosa la kuchelewa kufika sehemu ya
kurekodia filamu.
没有评论:
发表评论