2014年3月21日星期五

WANANCHI WA DRC WANAOMBWA NA CHAMA TAWALA KUSAIN WARAKA KUMTAKA RAIS KABILA KUWANIA TENA URAISI MWAKA 2016.

Katibu mkuu wa chama cha PPRD cha nchini DRC
Katibu mkuu wa chama cha PPRD cha nchini DRC
www.congosynthese.com

Na Sabina Chrispine Nabigambo


Chama tawala nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo PPRD kinaomba wananchi wa nchi hiyo na wafuasi wa chama hicho kusaini waraka maalum kutaka rais Joseph Kabila awanie tena urais nchini humo mwaka 2016.

Akizungumza kwa niaba ya wanachama wa chama cha PPRD cha rais Kabila wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho, Katibu mkuu wa chama hicho Claude Mashala amesema kuwa chama chake kimependekeza marekebisho ya katiba kwa sababu baadhi ya ibara za sheria zimepitwa na wakati.

Kwa mujibu wa katiba hiyo ya mwaka 2006, Rais Kabila anaelekea mwisho wa muhula wake wa pili na wa mwisho na hastahili kuwania tena urais mwaka 2016.

Wiki mbili zilizopita msemaji wa serikali ya Kinsasha Lambert Mende, alinukuliwa akisema kuwa rais Kabila hana mpango wowote wa kugombea kwa mara nyingine, kauli ambayo imetiliwa shaka na wapinzani wanaomtaka Kabila mwenyewe ajitokeze na kuzungumzia hatima yake.

Katiba nchini DR Congo inasema mabadiliko yoyote ya Katiba yanaweza kuombwa na Rais, serikali, bunge , au mchakato wa kukusanya saini elfu mia moja kama inavyopendekezwa sasa na chama tawala cha PPRD

没有评论:

发表评论