STAA wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amefunguka kuwa kama
siku yoyote atapata ujauzito kwa bahati mbaya, hatafanya kosa tena,
atazaa tu. Katika mahojiano maalum na gazeti hili juzikati, Lulu alisema
kwa sasa yuko tayari kuolewa ili awe na familia yake ila si kwa sharti
la mwanaume husika kumwambia amzalie kisha ndiyo amuoe.
Ijumaa: Kwani kwa sasa si una mpenzi? Lulu: Ndiyo ila bado sijapanga
swala la kufunga naye ndoa. Ijumaa: Kwa hiyo umesema ukipata mimba kwa
bahati mbaya hutofanya misteki lazima uzae, unaweza kuniambia ni misteki
gani? Lulu:
Nadhani
maswali yako uliyoniuliza nimekujibu kiufasaha kabisa hilo siwezi
kulijibu. Ijumaa linahisi kosa ambalo Lulu hatalirudia tena ni la kutoa
mimba, kitu ambacho hataki kukizungumzia.
没有评论:
发表评论