Ni vigumu sana kwa mtu wa kawaida
kupata nafasi ya kuingia kwenye chumba cha maandalizi au sehemu maalum ya
maandalizi nyuma ya jukwaa ya staa kama 2 Chainz na kuuza sura. Nafasi hiyo
aliipata msichana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Tina.
Msichana huyo aliingia kwenye chumba
hicho na kula pozi akiwa amepewa sapoti ya kufanya hivyo na watu wa karibu wa
2Chainz ambao alidai kukutana nao kwenye Instagram, lakini pia alijikuta
akipiga story na 2Chainz mwenyewe huku akirekodiwa katika video.
Baada ya maongezi ya dakika , watu
wa 2Chainz walimfahamisha kuwa kila kitu kinarekodiwa na kwamba hapo back stage
palikuwa ni sehemu ya watu wa blogs.
Msichana huyo alijiweka poa na
kuongea mawili matatu huku akijipa shavu kwa watu wamfuate kwenye Instagram.
“Aww sh*t! This is going on a blog,
for real?! This is going on a blog and you’re really recording? Do I look good?
You guys can follow me at Iluvtinaa on Instagram.” Alisema Tina huku
akiiangalia kamera.
Baada ya utani na kumpongeza 2Chainz
kwa show yake aliamriwa kuondoka eneo hilo.
Lakini baada ya 2Chainz kuiweka
kwenye mtandao video ya tukio zima mambo yaligeuka na msichana huyo hakupenda
kabisa jina ambalo video hiyo ilipewa, maandishi yaliyomtaja yeye kama kahaba
kwa neno ‘THOT’ (That H*e Over There).
‘#isthisYoThot’ iliandikwa video
hiyo.
Msichana huyo aliandikwa kwenye
Instagram kuwa amechukizwa na kitendo alichofanyiwa na 2Chainz na kwamba
anatamani 2Chainz angejisikia kama alivyojisikia vibaya na kudai kuwa
ameshaanza kufanya utaratibu wa kumfungulia mashitaka.
“Niko kwa
mwanasheria wangu muda huu, namalizia taratibu za kisheria, jiandae kwa kesi,
hauna haki ya kuvuruga maisha yangu na kunichafua kama hivi. Sasa wote mtajibu
kwa hili.” Ilisomeka sehemu ya ujumbe wa Tina kwenye Instagram
没有评论:
发表评论