Mwanafunzi mmoja wa Chuo
Kikuu Dodoma – UDOM aliyefahamika kwa jina la KAMUGISHA S/O ISACK, Miaka 24,
Mhaya, Mwaka wa Tatu, Kitivo cha
Sayansi ya Jamii (Social Science) anayeishi Block Namba 11, chumba Namba 62, alijitupa kutoka ghorofa ya pili hadi chini na kusababisha majeraha sehemu za mdomoni, shingoni na paji la uso.
Sayansi ya Jamii (Social Science) anayeishi Block Namba 11, chumba Namba 62, alijitupa kutoka ghorofa ya pili hadi chini na kusababisha majeraha sehemu za mdomoni, shingoni na paji la uso.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Dodoma Kamshna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME amesema tukio hili
limetokea terehe 18/03/2014 majira ya 20:15 huko maeneo ya chuo kikuu cha
Dodoma manispaa na Mkoa wa Dodoma.
Kamanda MISIME amesema uchunguzi
wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni ulevi. Majeruhi alilazwa katika
hospitali ya UDOM na baadaye kuhamishiwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma na kuruhusiwa
tarehe 20/03/2014 baada ya kuonekana hali yake inaendelea kuimarika.
CDT:Boss Ngasa Blog
没有评论:
发表评论