KILA jambo
na wakati wake! Hatimaye staa wa filamu za Kibongo, Blandina Chagula
‘Johari’ yuko kwenye mwanga wa maisha ya ndoa kufuatia Kiongozi wa Kundi
la Mtanashati, Ostaz Juma Namusoma kuweka wazi uhusiano wao wa
kimapenzi huku akisema ana mpango wa kumuoa kabisa, Risasi Jumamosi
linakupa zaidi.
Staa wa filamu za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’.
YAMEKUJAJE?
Hivi karibuni katika mtandao wa kijamii wa Instagram, Ostaz
alitumbukiza picha inayomwonesha yeye akiwa katika ‘pozi nono’ na Johari
huku akimsifu mwandani wake huyo. Hali hiyo ilisababisha maswali kwa
baadhi ya mashabiki wa Johari.
Risasi Jumamosi lilianzia hapo kuchimba hatua kwa
hatua na kubaini kuwa, wawili hao wako ‘klozidi’ tangu kitambo hasa
baada ya penzi bubu la Johari na staa mwenzake wa sinema za Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ kuparaganyika.
Kwa sasa Ray anadaiwa kutoka kimapenzi na mcheza filamu mwenzake,
Chuchu Hans ambapo nao inadaiwa wako katika mikakati ya kufunga ndoa
kama si pingu za maisha.
Johari na Ostaz Juma katika picha ya pamoja.
Chanzo chetu kimoja kilisema kuwa, Ostaz amekufa kimapenzi kwa
Johari, ‘hakohoi, hanywi maji, halali usingizi’ na yuko tayari kwa ndoa
itakayokuwa ya kifahari.
“Ukitazama hapo Johari hana kipingamizi, ingekuwa zamani angesema
yuko na Ray kuna kikwazo cha yeye kuolewa na Ostaz, lakini kwa sasa kipi
kitamzuia?” chanzo hicho kilipayuka.
MSIKIE OSTAZ
Baada ya kuzinyaka taarifa hizo na picha ya wawili hao kwenye
mtandao, mapaparazi wetu walimsaka mwanaume huyo kwa njia ya ujumbe
mfupi wa maneno (SMS) kupitia simu yake ya mkononi na mambo yalikuwa
hivi:
Risasi Jumamosi: Kaka kuna tetesi kwamba una uhusiano na Johari, unasemaje?
Ostaz: We nani?
Risasi: Mwandishi wa Risasi Jumamosi.
Ostaz: Ndiyo Johari ni wangu na mimi ni wake, tutafunga ndoa watu watashangaa sana.
Risasi Jumamosi: Huoni kama Ray atakukasirikia?
Ostaz: Kwani yeye ndiyo amemzaa Johari?
Risasi Risasi: Lakini kaka wewe mbona umeoa?
Ostaz: Mbona sikuelewi, Muislam mwisho ni wake wangapi?
Risasi Jumamosi: Vipi mkeo karidhia na lini ndoa?
Ostaz: Na Johari anataka kuslimu kuwa Muislam, tumepanga jina, ataitwa Rahma.
Risasi Jumamosi: Jambo jema. Mmeanza lini uhusiano wenu?
Ostaz: Hayo mengine muulize Johari mwenyewe mi nimeshasahau maana nina mambo mengi ya kujenga taifa.
“Lakini mimi nilianza na Johari kabla ya huyo Ray wenu, wakati huo
Johari akiwa anaishi Mburahati (Dar), yeye alikuwa anafanyia mazoezi ya
kuigiza pale TZF (baa), Kigogo.”
JOHARI SASA
Kutokana maelezo hayo ya Ostaz, Risasi Jumamosi lilimtafuta Johari kwa simu yake ya mkononi na kumuuliza kama kweli yu mapenzini na mfanyabiashara huyo maarufu jijini Dar.
Johari: “Hamna bwana, kama Ostaz mwenyewe ndo’
kasema hivyo huenda alikuwa anatania tu. Kweli hakuna kitu kama hicho,
ila ni mtu ambaye nina ukaribu naye mkubwa lakini si mapenzi.
Risasi Jumamosi: Kama ametutania mbona sisi siyo watani wake?
Johari: Mimi sijui sasa, yeye ndiyo anajua.
Risasi Jumamosi: Kama ni hivyo, wewe huoni kwamba utani wake ni mkubwa sana?
Johari: Mimi sijui chochote jamani, muulizeni yeye.
Baada ya kuzungumza na Johari, Risasi Jumamosi lilimgeukia Ostaz na kuulizwa kama kuna utani ndani ya maelezo yake.
“Jamani, ninyi mnachotakiwa kukielewa ni kuwa, Johari ni wangu na
mimi ni wake. Siku ya ndoa tutaitangaza, itakuwa ndoa kubwa sana na
Johari nitamfanyia mapenzi ambayo hajawahi kufanyiwa tangu azaliwe.”
WASEMAVYO MASTAA KUHUSU JOHARI NA OSTAZ
Baada ya kumalizana na wawili hao, Risasi Jumamosi liliwatafuta
mastaa wa filamu za Bongo ili kusikia kutoka kwao wanachokijua kuhusu
Johari na Ostaz.
Mastaa waliopatikana ni watatu, lakini wote walitoa ushirikiano kwa sharti la kutoandikwa majina yao gazetini.
WA KWANZA, MWANAUME:
“Khaa! Mbona siyo siri, kwani nyie mmejua lini? Wale wako tangu
zamani sana tena wengine mpaka tukadhani walishaachana, kumbe bado wapo
pamoja?”
WA PILI, MWANAUME:
“Oohooo! Mlikuwa hamjui? Wale ni wapenzi. Mimi ninavyojua wana mpango
wa kufunga ndoa lakini sijui ni lini na Johari atabadili dini.”
WA TATU, MWANAMKE:
“Mh! nilishasikiasikia, unajua Johari ni msiri sana, hajawahi kuweka wazi lakini ni kweli wana uhusiano wa kimapenzi.”
KAMA NI KWELI, CHEKI SINEMA YAKE
Endapo ni kweli Johari atabadili dini, ina maana atakuwa amekwenda
sambamba na Ray kwani yeye anadaiwa kubadili dini kwa ajili ya kumuoa
Chuchu Hans, Johari atabadili dini ili aolewe na Ostaz
没有评论:
发表评论