2014年3月27日星期四

MLINZI WA RAISI OBAMA AMEFUKUZWA KAZI BAADA YA KULEWA BWII AKIWA KAZINI.

 
Jarida la Washington Post nchini Marekani limeripoti kwamba askari watatu ambao ni walinzi wa president wameachishwa kazi kwa muda na kurudishwa nyumbani ili uchunguzi ufanyike.
Askari mmoja kati ya hao alikutwa amelewa pombe chakari kwenye hoteli moja huko Amsterdam ambapo Obama alienda kwa ajili ya mkutano wa mambo ya Nuclear.
Msemaji wa idara ya upelelezi Marekani alikataa kutoa taarifa zaidi kuhusu tukio hilo ingawa alisisitiza kuwa watatu hao wameachishwa kazi kwa muda huku uchunguzi ukiendelea.
Mwaka 2013 majasusi wawili waliondolewa katika kikosi cha ulinzi cha Rais Obama kufuatia tuhuma za kuhusika na kashfa ya ngono na utovu wa nidhamu.
Mwaka 2012 majasusi kadhaa waliachishwa kazi kufuatia madai kuwa walikodi makahaba walipokuwa mjini Cartagena Colombia

没有评论:

发表评论