Kama inavyofahamika kampuni ya Weusi ilikuwa inaunganisha rappers wa makundi mawili ya wanajeshi wa muziki mzuri toka Arusha, Nako 2 Nako Soldiers na River Camp Soldiers.
Kufuatia uamuzi wa Weusi, G-Nako ameeleza mtazamo wake pia kwa kuzingatia kuwa yule ni mwanafamilia mwenzake wa kundi hilo.
“Nafikiri alichokwambia Nikki ni kitu ambacho tumekubaliana watu wote na msimamo kama wa kampuni ndio huo.” Amesema G-Nako. “Haijalishi kama ni member, ni Nako 2 Nako ni nini lakini Lord Eyez ni mmoja wa wanahisa wa Weusi na kilichofanyika ni hicho na maamuzi ndio hayo, hilo swala liko ndani ya Kampuni.”
Baada ya Lord Eyez kusimamishwa kazi, hivi sasa Nako 2 Nako ina mwanahisa mmoja tu kwenye kampuni ya Weusi, huku wana River Camp wakiwa watatu. Biashara inaendelea na sheria inafuata mkondo.
Hata hivyo, bado kuna mkanganyiko kati ya tafsiri ya tamko la Weusi kwa baadhi ya watu, ambapo wengi wamechukulia ‘kusimamishwa’ kama ‘kufukuzwa’
. Hii imempelea Joh Makini kufafanua.
“Lord Eyez hajafukuzwa wala kutengwa kama wengi mnavyoitafsiri.” Joh Makini ameandika Instagram na kupost picha akiwa na Lord Eyez
没有评论:
发表评论