“Sifahamu hizi tetesi zimetokea wapi. Nilikutana na Diamond mara moja, na ilikuwa wakati tunarekodi wimbo wa ONE Campaign Afrika Kusini wiki mbili zilizopita.” Victoria Kimani aliiambia Nairobi News.
Aliongeza kuwa hata hawajawahi kuwasiliana kwa simu tangu walipomaliza kupiga picha hizo na zaidi hata namba ya Diamond hana.
“Hata sina namba yake, kwa hiyo sijawasiliana nae tangu tulivyokutana Afrika Kusini.”
Hivi karibuni kaka yake Victoria Kimani, Bamboo alitoa maoni/mtazamo yake na kudai kuwa Diamond sio ‘type’ ya Victoria Kimani.
Hata hivyo, Diamond alikuwa wa kwanza kuzikanusha tetesi hizo na kudai kuwa mrembo huyo ni mshikaji wake tu
没有评论:
发表评论